Incoterms ni masharti ya biashara yaliyochapishwa na Chama cha Kimataifa cha Biashara (ICC).
Masharti haya yanatumika katika mikataba ya kibiashara duniani kote kufafanua majukumu na dhima ya wauzaji bidhaa nje, waagizaji bidhaa, na wahusika wengine kama vile wasafirishaji, watoa bima, wafadhili na wanasheria wanaohusika katika shughuli ya biashara. Incoterms huweka mipaka ya muda/mahali ambapo msambazaji ataacha kuwajibika kwa bidhaa na mnunuzi kuchukua madaraka.